Virusi vya Korona na Kristo - Epub

Virusi vya Korona na Kristo - Epub

Mnamo Januari 11, 2020, virusi vipya vya Korona aina ya SARS-COV-2 vilitangazwa kwamba vimeua mtu wa kwanza katika mkoa wa Wuhan nchini Uchina. Mnamo Machi 11, 2020, Shirika la Afya duniani lilitangaza ugonjwa wa Virusi vya Korona kuwa janga la kimataifa.

 

Katika hali ya hofu na wasiwasi, ni kawaida kwa mtu yeyote kuuliza, “Kwani Mungu anafanya nini katika hali hii?”

 

Katika kitabu cha ‘Virusi vya Korona na Kristo’ John Piper anawasihi wanaosoma kitabu hiki katika ulimwengu mzima kusimama juu ya Mwamba imara, ambao ni Yesu Kristo. Ni hapo tu ndipo roho zetu zitapata kuendelezwa na Mungu mwenye mamlaka. Yeye ndiye aamuruye, asimamiaye, na atawalaye vitu vyote ili akamilishe makusudi yake ya hekima na mema kwa wale wamwaminio.

 

Mwandishi wa kitabu hiki John Piper anatoa majibu sita ya kibiblia kwa swali, “ Mungu anafanya nini kupitia kwa Virusi vya Korona? – akitukumbusha kwamba Mungu anafanya kazi wakati huu wa kihistoria.